Mwongozo

FAQs

..Nini madhumuni ya Blogu hii?
Blogu hii imeandaliwa kwa madhumuni ya kuwarahisishia wapenzi wote wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama 'Bongofleva' kupata mashairi mbalimbali ya nyimbo wazipendazo, kwa kuomba (request) mashairi ya nyimbo husika au kutafuta kati ya mashairi yaliyokwisha chapwa.

Natoaje maoni?
Ili kutoa maoni au ushauri kwenye blog hii huna budi ku sign in kwa akaunti yako ya Facebook. Wakati mwingine sehemu ya kutolea maoni inaweza isionekane, inapotokea hii jaribu ku 'refresh browser' yako au ku'load page upya.


..Vipi kuhusu usahihi wa Mashairi?
Kadiri ya uwezo wetu tunajaribu kuchapa mashairi kwa ufasaha, ila pia kumbuka kulingana na aina ya wimbo, wakati mwingine ni vigumu kusikia kila neno litamkwalo/ kwenye nyimbo husika. ndio maana basi, tumeweza kuwezesha kijisanduku cha maoni ili uonapo kwamba mashairi yana makosa uweze kutoa maoni ili tuweze kurekebisha sehemu husika..hatuwezi kukuhakikishia kwamba mashairi yote uyasomayo hayana makosa.


...Je kuhusu Viunganishi (Links)?
Mtumiaji aelewe kwamba blogu hii inaweza kuwa na viungo (external links) za kwenda kwenye tovuti tofauti, wamiliki wa blogu hii hawapo tayari kwa malalamishi yeyote yatakayotokana na utumiaji wa blogu hizi, zingatia kufuata taratibu na sheria za tovuti/blogu husika.


...Naweza kupakua(Download) MP3?
 Kwanza tambua upakuaji wa nyimbo au MP3 za wasanii husika ni uvunjaji wa sheria, na pia kwa kufanya hivyo unawadidimiza na kuwanyima haki ya msingi ya kunufaika na kazi zao, kwahiyo kumbuka hatutunzi wala kuhusiana na viunganishi (links) vya nyimbo zozote zilizo kwenye blogu hii na hatuzihifadhi kwenye mfumo (database) yetu, nyimbo zote ni kutokana na viunganishi (hotlinks) kutoka sehemu mbalimbali mtandaoni



...Nifanye nini ninapohisi hatimiliki yangu imevunjwa na MB?
Ni matumaini makubwa ya wanaohusika na blogu hii kwamba watumiaji wote, binafsi au mashirika watafuata sheria zote za hatimiliki. japokuwa, tutakapo pokea malalamiko yeyote yanayohusiana na uvunjaji wa hati miliki kutoka katika kampuni au wasanii binafsi, tutaondoa mali/kazi ya msanii au kampuni husika katika blogu hii haraka iwezekanavyo lakini pindi tu pale tutapobaini na kuwa na uhakika kuwa mlalamikaji ni mmiliki halisi wa kazi hiyo.

..Tunayapokeaje malalamiko?
wanaohusika na blogu hii wapo tayari kufuata hatua za kisheria na hawataingilia mfumo huo pindi watambuapo hatua hizo ni za kimsingi na zipo chini ya sheria za hatimiliki husika. Tutumie email au bofya hapa kutoa malalamiko yako..


Mashairi101@gmail.com
Tutafute pia kupitia google+ [Mashairi bongoflava]