Ya moto Band - nitakupwelepweta

Unajifanya bingwa wa kupenda...dada ee
Kumbe bingwa wa kutenda kuliko kupenda ..dada ee
Tena unasifa yakuogopwa kama difenda.. dada ee
Umeua wengi ila kwangu umedunda
Ahh koma ee sitaki nizikwe na kilo mbili kwenye mfuko
Mama eee sitaki familia ilie kwasababu yako
Dada eee ananitegemea Mama ee...aeee
Nikifa atalia sana...eee aa
Katika familia na mimi ni baba japo baba yupo
Nikija kufa ufa nani ataziba ebu kwenda zako
Ananitegemea mama ...ee aeee
Nikifa atalia sana...ee

Kuku wa kizungu mchinjaji ana tabu
Kuku wa kizungu mchinjaji ana tabu
Ebu niache..eh
Ebu niache unapita na dumu la petroli ebu niache
Ebu niache...eh
Ebu niache unapita na dumu la petroli ebu niache
Una rambo mi nina mua mi ujinga ujinga tu Eee hujaniua
Una rambo mi nina mua mi ujinga ujinga tu Eee hujaniua

Unakichaa mimi nakuita wewe mwendawazimu
Nimepata habari mwili wako umeujaza sumu
unang'ang'ana unataka mm kunipa utamu
umekosa sengeru ngoma ya kucheza huna nenda kaicheze

Segere,segere mamasegere segere ohhhh
segere segere Mama
We mwali nenda kaicheze

Segere,segere mamasegere segere ohhhh
segere segere Mama
We mwali nenda kaicheze

Mama mama mama mamaa
Eti ametuma mashoga zake waje kuniambia
Roho inamuuma kidudu penzi kinamsumbua
Siri imevuma mimenyula wengi wanajipakua
hana huruma kalitoa wapi aje kuniua
Ilikuwa siasa nikatoa nikagawanya
nikajua anadanganya we m'baya wee
Nusu dengu Nusu dona wengi wao unawadanganya
Mama chidi we kitanda huna haya weeee

Mimi si saizi yako nitakupwelepweta bure
Tafuta taipu yako wa ilala mm wa kilungule

Mimi si saizi yako nitakupwelepweta bure
Tafuta taipu yako wa ilala mm wa kilungule

Unataka kunipepelusha we kimbunga huniwezi ng'oo
kina chako cha maji marefu kuogelea sikiwezi ng'oo
Unashinda kuwinda vyenye kung'aa vya masizi
huvitaki noo
Unang'ang'ana kama ruba kwenye mwili wangu
we nenda zajo yeee
Na ushindwe ushindwe uniache mm mwana wa mwenzio
kwetu ndo jembe jembe ukivunja mpini ni kilio

Unakichaa mimi nakuita wewe mwendawazimu
Nimepata habari mwili wako umeujaza sumu
unang'ang'ana unataka mm kunipa utamu
umekosa sengeru ngoma ya kucheza huna nenda kaicheze

Kuku wa kizungu mchinjaji ana tabu
Kuku wa kizungu mchinjaji ana tabu
Ebu niache (Eeh)
Ebu niache unapita na dumu la petroli ebu niache
Ebu niache (Eeh)
Ebu niache unapita na dumu la petroli ebu niache
Una rambo mi nina mua mi ujinga ujinga tu Eee hujaniua
Una rambo mi nina mua mi ujinga ujinga tu Eee hujaniua

Ana chuma cha moto huyoo
Anaunguza watoto huyooo
Apewe mkong'oto huyooo
Ili ifike mwisho huyooo
tabia yake,tabia yake,tabia yake