ah
beat kali haifai bila vocal
daily nakula dry, niko high kama popo
fanya worldwide so ku-try kama local
fake emcee ukijikoki mi na squeeze kama .44
ah verse baridi vaa koti
Salamu kwa wanangu wote sina report
bado misheshe support mwanangu OP
Kila beat natoboa kama juice ya kijoti
ni discipliner nawasimamisha wima
mi nyarapa mpaka sura kama simu ya kichina
mistari ina vina, kwenye shari habari sina
mchaga halali macho kwenye salary daima
zunguka kote hauna rafiki kama noti
sistaduu hauna mnafiki kama shosti
tafuta dili uza hata pipi we bitozi
tafuta njia haya maisha hayamuliki kama tochi
chapchap, chapchap ni sawa
Mlab pure math, rap ni dawa
chapchap, chapchap ni sawa
Pure mathematics, dogo utapagawa/utachachawa
ah
we unachana mi ninachana mpaka basi
niko booth nina biki karama na karatasi
sina hofu nina speak salama kwa sala safi
ila ukinivaa vibaya nakuchana kama vazi
sanaa. gharama haramu chati
harakati hii kubwa hupaswi simama kati
verse inacheza judo, kata na sarakasi
baba mama mbarikiwe kusimama ka wazazi
pure number, hapa zinajamba za kubuni
mshamba kawa mjanja, mjanja ana ujanja wa kihuni
m banje kwenye beat weka ladha ya sabuni
we ni base ten log mi ni namba ya kirumi
hii ni classic, hata isipotamba kama 'do me'
kasi ya marapper inasanda kama uchumi
nina punchlines na kick kama chuo kikuu cha ngumi
pure mathematics sina banda nina kampuni
so
chapchap, chapchap ni sawa
Mlab pure math, rap ni dawa
chapchap, chapchap ni sawa
Pure mathematics, dogo utapawa/utachachawa
kuna rapper mwenye akili na rapper batili
rapper anayepata akisaka, na asiyepata akisaka dili
tofauti kati ya rapper wa kwanza na rapper wa pili
wa pili anataka u master huku hajapata umahiri
fungua ukurasa kwenye darasa la hip hop somo
halisi tunaoandika kusikika inataka promo
midomo inasikika ikisema na mikono inashika
makoleo na kuzika waliomo
waliopotea njia wanataka kurudi nyuma
wapotovu wamechuna, waovu wamenuna, inawauma
wamepoteza mwelekeo maendeleo yamegota watafanya nini leo
panapo matatizo tunataka suluhisho
likizo inawekwa kando tunakaza mpaka kifo
na tulivyo, sio watu wa matambiko
tumeshaiteka kambi na kupekua maficho
so
chapchap, chapchap ni sawa
Mlab pure math, rap ni dawa
chapchap, chapchap ni sawa
Pure mathematics, dogo utapagawa
chapchap, chapchap ni sawa
Mlab pure math, rap ni dawa
chapchap, chapchap ni sawa
Pure mathematics, dogo utachachawa
ah
[Mashairibongofleva.blogspot.com]