Stamina ft Fid Q - Wazo la leo

you know what majani?
nice to meet you homie!

yeah
elimika nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo
Pesa ni vazi la ngema, haliwezi kuwa na mpasuo
vaa uaminifu, tupa boksi la kondomu
Hip Hop haijengwi na beef, underground usiijaze form
maisha ni kujipanga, ewe mganga usigawe hirizi
viogonzi msiizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa lease
ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti
mkulima rudi shamba, nahisi mbegu siku hizi hazioti
maisha njia panda, mtembezi chagua pa kwenda
uchumi vazi la bwanga, ukishuka uvishe suspender
shiba kwa nia, ukiwa mrefu wa malengo
usikufuru we shukuru, ukifaulu kila tendo
punguza pupa, mpendaji uingie ndoani
mapenzi yamevaa bukta usiwaze, mapaji hadharani
usilale kijinga kwenye kitanda cha ushamba
unaweza kuwa shabiki wa simba na ukaishi mwembe'yanga
ah

hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
neno la kuponya, lililokosa mdomo
na hili bonge la ngoma kwenu, kwangu ni kama somo

hilo ndo wazo la leo, ishi usingizi wa furaha
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha
Hilo ndo wazo la leo
usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo vyako
Hilo ndo wazo
ah

underground panga tenzi, u'star hauji kwa promo
hakuna tajiri wa mapenzi, kapuku punguza ngono
bora uuitwe Mfalme Juha, kwenye utawala wa kishamba
mapenzi yakikusumbua, tafuta daktari wa kitanga
vazi unaloishi,mwenyezi yeye ndo Designer
shetani akikushawishi, mvute kwake kama Dyna
Dunia duara, jitahidi uizunguke
mla bata starehe hasara, wekeza hadhi isishuke
huna undugu na Bakhresa, ni aje aje unakula unga?
Mateja mnahitaji sensa, taifa la kesho linavunda
Dogo jifunze heshima, sio upaparazi
mwambie na dada ajitunze, mlango wake asiuache wazi
kama unajijua ni mchoyo, basi usingonje kupewa
tafuta pesa kwa moyo, sio kwa ushindi wa ngekewa
Sharo mpe salamu, The Great braza Kanumba
Mwambie bongo sio tamu, na Lulu bado wamemfunga

hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
neno la kuponya, lililokosa mdomo
na hili bonge la ngoma kwenu, kwangu ni kama somo

hilo ndo wazo la leo, ishi usingizi wa furaha
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha
Hilo ndo wazo la leo
usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo vyako
Hilo ndo wazo

utamu wa ndafu ya harusi, sio wa ndoa we kilaza
mbuzi atabaki mbuzi, hata ule hadi ukasaza
nchi tayari imekonda, mwananchi tafuta ulaji
life ngumu hadi ombaomba, kidonda anafanya mtaji
ukipata mazuri, jipange kukwepa hasara
kijana vazi la msuli, haliwezi 'kuvisha busara
ukiishi kwa hisia, kila story litakubanza
cha msingi kuweka nia, ujivunie kuwa Mtanza(nia)
kata ya kijiji, haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mgwiji, msuli ukishuka kimeo
uchumi unashika tama kwenye shavu la mlanguzi
Raia usilaumu chama, shiriki kwenye uchaguzi
unaweza kuvaa kinga, ila ukafa kwa uaminifu
mzinzi usigawe ujinga, sambaza ujumbe wa sifa
hakuna snitch kama pesa, ukiwa naye fanya vya maana
akiondoka atakutesa, utamsaka usiku na mchana

hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
neno la kuponya, lililokosa mdomo
na hili bonge la ngoma kwenu, kwangu ni kama somo

hilo ndo wazo la leo, ishi usingizi wa furaha
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha
Hilo ndo wazo la leo
usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo vyako
Hilo ndo wazo
ah

[Mashairibongoflava.blogspot.com]