Kwengine sitamani, ile ahadi uliyonipa moyoni
nahisi ni shetani, aliyenibadili mawazo kichwani, mh
ona mapenzi ni mfalme hadundwi, nimezama ni vigumu kutoka
ona nakesha ni kama bundi, nikilala kuna kitu nakiota
umenipa upofu 'ngali hai mboni zangu, unaniumiza
ukanipa donda ndugu moyoni mwangu, maumivu yalopitiliza
umenipa upofu 'ngali hai mboni zangu, unaniumiza
ukanipa donda ndugu moyoni mwangu, maumivu yalopitiliza, ah
mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
mbona, mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ah ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
ningekunywa pombe ili nipunguze mawazo lakini siwezi
nahisi kama ndo nitazidisha mawazo na maumivu ya mapenzi
mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
mbona, mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ah ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
uhh uhh uhh
rudi nyumbani, rudi nyumbani
uh tuishi wawili, tujenge family
uh rudi nyumbani
uh rudi nyumbani
mzizi wa mapenzi moyoni, umekata kwa kinywa chako
huwezi kujua machoni, kama nime'miss pendo lako
ona macho yangu yalivyonyauka, kwa kutazama penzi linalozamia
mmh nimechoka kulamba, nahisi kama unanionea
mimba za hisia na mawazo, kichwani bado zinajitunga
ninapojiuliza nini chanzo, naumia naona bora kuimba
wanipa tabu ya kusafisha kaniki, wakati rangi inajulikana
mmh nashindwa usingizi sipati, nakosa raha usiku mpaka mchana
mhhh, hey hey
mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ah ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
ah ona, mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ah ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
ningekunywa pombe ili nipunguze mawazo lakini siwezi
nahisi kama ndo nitazidisha mawazo na maumivu ya mapenzi
mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ah ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
ona, mbona silali, kisa mawazo mwenzako sili
ah ona, watoto nyumbani, wanauliza wapi mami
uhh uhh uhh
rudi nyumbani, rudi nyumbani
uh tuishi wawili, tujenge family
uh rudi nyumbani
uh rudi nyumbani
[MashairiBongoflava.blogspot.com]