[ina mi yard....keeping the good music alive]
amen, amen
amen, amen
Mungu Niongezee!
amen, amen
amen, amen
Nishike mkono niongoze
On and on kama Erykah Badu, wafahamu sababu
ni heshima kwa mungu
Natembea kifua mbele, yote sababu ya wewe
wote wanaojipindua mwisho wanasanda wenyewe
Binamu yangu nazunguka na huu mziki hata nikiwa jela
Jinsi nakinukisha na bado juhudi na sala
naomba hekima za Suleiman, sio minguvu ya bure
hata kauli zangu ndogo, zionyeshe nilienda shule
adui wafunge midomo, nini nimewazidi wape ishara
wape akili za hasara, wachezee kazi na mshahara
ikidunda sana inakaribia kupasuka
yangu kesho isiishe leo, hata wajukuu wanaikuta
bora kuchekwa, kuliko kuchekwa sana
wanaonipinga waumize, Mungu nakuomba sana
uwape umri mrefu, wa kwangu na wababu yangu
ili roho zao ziumie wakiona mabalaa yangu
amen, amen
amen, amen
Mungu Niongezee!
amen, amen
amen, amen
Nishike mkono niongoze
nisichokijua hakiwezi kunisumbua
wakisema mabaya, yashindwe kunifikia
wape kismati cha paka, cha kupendwa na wachawi
mi naomba cha pesa, na kwa ujinga niwe kiziwi
wape wanawake wazae na mafukara, halafu wagonjwa
ama mabwana mabwabwa wasiogonga kabla ya kugongwa
wanaomba nisiwe na kitu, ili niombe waninyanyase
dhiki inijae, vyote vya kwangu wavipate
kuna viumbe hata uwajui, na bado wana beef na wewe
kama wanichukue msukule, nisionekane wabaki wenyewe
naishi kwa kudra, baraka matakwa yako siwezi nikachemsha
kama ukibaki upande nilipo
competition is irrelevant, with you by my side
ntafanya siongei, na unajua mi ni master
madaraka zaidi yao, uchungu zaidi yao
ukubwa udogo wa tatizo unaletwa na akili zao
amen, amen
amen, amen
Mungu Niongezee!
amen, amen
amen, amen
Nishike mkono niongoze
[Mashairibongoflava.blogspot.com]