shida zinaomba urafiki, umaskini unaleta posa
ukubwa meli ya kigiriki, umezamia bila boxer
bikra wote wameshavunjwa na balehe
ukubwa una mingi misoto, na mchangaji wa starehe
mara oh baba kijacho eti niandae hela ya nepi
wife anatoa macho, anangoja shopping ya sketi
hakimu ana nyundo ya noti, mtuhumiwa anasaka chenji
bongo mahakama za joti, mi mpoki nabaki benchi
hata nikimchukia baniani kiatu chake hakina mchango
mzinzi na nyota ya kijani, ndo uzazi usio na mpango
kubalehe noma ka baunsa aliyepigwa na mtoto
ukubwa mechi ya kisodoma, haiwezi chezeshwa na mpoto
ah, kasi na kasi ni kasi isiyokuwa na kasi
ila nikiweka kasi na kusi, ndo kusi pacha wa kasi
bora wewe jalala mi ukubwa shimo la choo
ukichanganya na ufukara ndo mechi isiyo na droo
ah
kama nakufuru mungu naomba unisamehe
nakosa uhuru sikumbuki hata tarehe
kweli najuta kuzijua hizi starehe
hey, mi najuta kubalehe
hey, sikumbuki hata tarehe
hey, ujana maji ya moto zinaniunguza hizi starehe
maisha ngumi ya bitozi siogopi kutega sura
pesa sitafuti kwa pozi, bado najinyima kula
nishachoka kusadiki, tomaso tangu na tangu
marafiki wanafiki wana'snitch hadi kwa mke wangu
majukumu ya familia, nimeyabeba bila ngata
siri zimezidi mia, desturi zimenikamata
ya maumivu ya mjeledi, kwenye ngozi ya mlemavu
ukubwa mechi ya mabaamedi, mi mlevi nafungwa kavu ah
maisha jabali, ugomvi wa Cheka na Tasu
sikuhizi ukinunua hata ka-gari, kitaani unaitwa Freemason
maumivu ya sufuria, jikoni hayana ushuru
pesa tajiri wa dunia, mwenye saa yangu ya uhuru..aisee
siasa imenekera, ukwaju umenipa msoto
mtu mzima bila hela, utamuamkia hadi mtoto
nnapopata mkwanja na shida zinagonga hodi
vipi ntanunua kiwanja huku bado nadaiwa kodi
ah
kama nakufuru mungu naomba unisamehe
nakosa uhuru sikumbuki hata tarehe
kweli najuta kuzijua hizi starehe
hey, mi najuta kubalehe
hey, sikumbuki hata tarehe
hey, ujana maji ya moto zinaniunguza hizi starehe
ukubwa msafara wa kenge, mi mjusi vipi unichoshe
penzi kitovu cha uzembe nakaza nisiitwe Ngoswe
Ugangster bila hela, majibu yake ni uchafu
maisha ya bongo msosi wa jela, so mfungwa usiulize ndafu
nilizoea kashata bumunda na vibagia
huku unga bangi na bapa ndo vitu ninavyovisikia
chuki na fitina hazina za wenye wivu
wapo wenye ushirikina ili moto nigeuke jivu
udogoni nilidekezwa, wazazi walinipa malezi
pesa nimesomea udereva inaendesha hadi mapenzi
elimu ya njia za panya inanikosesha michongo
madeni yananiandama ka serikali ya bongo
maishani ukiwa govinda wenzako watakuita Yahaya
pesa mnyama anayewindwa na jangili aliyevuta kaya
wazi unanidondosha, bado narusha kombora
kondomu ndo kinga tosha sijikingi na bastola ah
kama nakufuru mungu naomba unisamehe
nakosa uhuru sikumbuki hata tarehe
kweli najuta kuzijua hizi starehe
hey, mi najuta kubalehe
hey, sikumbuki hata tarehe
hey, ujana maji ya moto zinaniunguza hizi starehe
heri ningerudi utoto, ujana maji ya moto
hey hey hey hey
[Mashairibongoflava.blogspot.com]