Chidi Benz ft Matonya - Usinipe lawama


Mami usinipe lawama
kama kukupenda baby, kwako nilizama
Mami usinipe lawama
kama kukupenda baby, kwako nilizama

ah
sipendi kukuaga, lakini sasa inabidi
siwezi kubali, mi unitese zaidi
kuwa free, kwangu usirudi
ingawa nilikupenda, ila tena sina budi
sikusemi vibaya, sikupigi mikwara
sIkutoi na ngumi, wala sikupigi ngwara
roho inaniuma ila najikaza kiume
na izuia akili pia vibaya nisikuume
najua utapendwa we sio mbaya mrembo
pozi unavyojiita we, kama naomi campell
ila tatizo tabia, kweli hujatulia
na, sijui wenzangu wataweza vumilia
labda, labda
ila mi nimeshindwa, nimevumilia sana
lakini uhuni wako umenishinda
nakukataa, ingawa bado nakupenda
nakuombea heri, popote tu utapokwenda

Mami usinipe lawama
kama kukupenda baby, kwako nilizama
Mami usinipe lawama
kama kukupenda baby, kwako nilizama

ah
nilikupenda sikupenda nikudhuru
sikuwa na wasi nilikuachia uhuru
ukicheche nilikuwa muoga ka kunguru
sikupenda, gombea niliogopa utuzuru
kumbe, kiguu na njia, changa la dunia
ninajua fifty-fifty kumbe mwenzangu we mia
nikipita natizamwa mi najua umependeza kumbe
story zako zinawafanya kunibeza
umeshindwa kustahamili, ukataka mawili
umetuzungusha kibao mzunguko wa tairi
nenda kawasulubu na, wengineo pia
mimi, niache nitafute atakayetulia
atakayenipenda, kweli asinitose
atakayeni'care asinifanye niogope
ingawa sitomjua ila naamini nitampata
wa tofauti kabisa asiyependa matata

Mami usinipe lawama
kama kukupenda baby, kwako nilizama
Mami usinipe lawama
kama kukupenda baby, kwako nilizama

ni wewe, uliyenipa kiwewe
mwenyewe, nataka unielewe
sasa vipi leo unione wa thamani
au kisa nna madini shingoni

ni wewe, uliyenipa kiwewe
mwenyewe, nataka unielewe
sasa vipi leo unione wa thamani
au kisa nna madini shingoni mimi

ni wewe, ni wewe
mami, ni wewe
kama kukupenda baby, kwako nilizama


[Mashairibongoflava.blogspot.com]

Sign in kutumia akaunti yako ya Facebook kisha comment!