we kushoto mi kulia, mtaani walitushuhudia
unapoonewa lazima nitaingilia ndivyo
ilivyokuwa na kwa upande wako pia
ulinipa moyo, na maneno mazuri
muziki sio bagamoyo ila tu nikaze msuli
nimuombe mungu, nisiache kusali
ipo siku tutawapiku tu wanaoendesha magari
rafiiki wa ukweli, maisha yangu uliyajali
ulisema niwe makini kuna ugonjwa hatari
nimheshimu demu wangu,
ukasema yule yule ndo ningefunga naye pingu
ukasisitiza kamwe nisije kumuacha siku,
nitayomwacha na ushkaji wetu utakwisha
love na peace, mchizi wa uhakika
kwa mdomo hadi maandishi mtaani ulikubalika
haukuwa mbishi,
kama ilivyo sasa unashinda na nguo mbichi
na unaonekana ka kibaka
ulikuwa smart bonge la mtanashati
leo upo vagaranti yote sababu ya Blunt
hauna noma na hauko safi kama wafuasi
waliojitahidi kukuokoa halafu wewe ukawa crash
ukawaona wabaya, kumbe unajisaliti kutwa nzima na kaya
ushauri wao hautaki, haulali nyumbani
ukionekana usiku tu unachungulia uani
mwana umenipa mtihani, kwenu wanajua upo kwetu
kwetu haupo hawaniamini, nafanya jitihada kondoo urudi kundini
ajabu maskani kwenu wote wananishutumu mimi
wanasema mimi ndiye, nnayekudatisha
wanasema mimi ndiye, ninayekupotosha
nimekutorosha hadi unalala kwa mapusha
na unaviwasha tu viarusha
Ja'mangu, yes! ungenisikiliza yote yasingekutokea
Ja'mangu, yes! ona nimekaa kimya kilichokuja tokea
Ja'mangu, yes! ungenisikiliza yote yasingekutokea
Ja'mangu, yes! ona nimekaa kimya kilichokuja tokea
Mtaani story ndo hizo mwana umepatwa na nini
wanataka waambiwe chanzo baadi yao hawaamini
maana, hata demu wako ananiuliza ulianza lini
ile kitu hutumii labda umekumbwa na jini
unakumbuka shule ulianza kama masihara
day moja nilikuotea class na pakti ya sigara
ukajitetea kuwa unafanya biashara
leo umesha use bang kila kitu kwako hasara
umeshachange life, umeshakuwa dhaifu
unajifunga mgwiji, kiunoni bonge la knife
unajichora tattoo majina wake za watu
mchana kwako usiku usije kugeuzwa ndafu
umekuwa wa mabifu, chuki na kila mtu
inanihuzunisha,
nikikumbuka maisha ya shule ndo yanasikitisha
hesabu sio sana ili Geography ulikuwa kichwa
ukanihidi hata ndege siku moja utakuja kuirusha
umepoteza future, ndege tena hutoirusha
kichwani umejaa moshi hata baiskeli tu unaangusha
mama analia, mwanaye anaumwa hakuna wa kumsaidia
ni nia yangu ni nzuri ila tu hamjanistukia
maana chali watu fulani washasema wanakuharibia
kwa nguvu napinga, mi nakujali mwanangu
na nakupenda si unaona niko peke yangu na demu wako amekutenga
anakuona kenge, akiulizwa anadai hakufahamu hata chembe
ila mwana usikonde, ingawa home utata wanajadili wapi uende
wengine kwa mgangaa, wengine mirembe
wengine labda kakobe aje home aombe
utapona usikonde
Jamangu, wewe wewe wewe
Ja'mangu, yes! ungenisikiliza yote yasingekutokea
Ja'mangu, yes! ona nimekaa kimya kilichokuja tokea
Ja'mangu, yes! ungenisikiliza yote yasingekutokea
Ja'mangu, yes! ona nimekaa kimya kilichokuja tokea
[MashairiBongoFlava.blogspot.com]
Sign in kutumia akaunti yako ya Facebook kisha Comment!