One the Incredible - 40 Bars


yeah
One take uno
duke touches
Mlab
One take uno
yeah

Habari noko, nina habari moko, 
huwezi timiza kazi, kama askari choko
juu ya daftari ninatafakari msoto,
 kwa mistari mitamu kama cadbury cocoa
hii ni classic move kama dansi, 
nawapa hisia kali zaidi ya movie za mikasi
kwenye chart zao wao washindani mi nafasi sifanani nao, 
mimi ni zao wao ni nyasi
mwanaharakati ka kikosi na si hasi,
 mistari ina siri nzito kama box la risasi
sipo cocky nipo confident, conscious reactions
kwenye booth niko lost kama park ya Jurassic, 
Genius niliyefeli kupass mathematics
kama rap ni drug mi nna habit kama addict, 
spit kama rabbit kwenye 8 mile love it or hate it
hardly debated hii ni 8 time classic
verse balanced ka account ya Fisadi, 
kwako mlevi wa u star kama round za vinywaji
dunda kavu ama bounce na kinywaji, 
skia biashara kwenye spika naita sound za miradi
nina ujumbe mtamu kama sound ya king'asti, 
snitch ask around niko down na illmatics
na spit kwenye mic ka risasi niko kasi, 
so huwezi pass around ka upo stuck kwenye traffic
ah, sibutui nashoot kasi tu huijui siku zote vipi unisumbue kilaza 
mdundo mweusi nausugua kama na msasa, 
mpaka duke ateme slang kama muvi ya ki hustler
hii kwa wote wanaeikubali, sio fulani na fulani aipende, 
mie ndo moko mukatano ya mistari ka stendi ya mwenge
fanya wengi waende mbali waache wachache wakae kizembe,
 kaa mbali nasi au kaa sawa nikulenge
sa kaa sawa snitch mi ni dawa kama jeezy, 
hawa wanahisi ila wako sawa kama sisi
na kama mkavu hapa utanawa utakuwa mbichi, 
money ni power respect unaipata ukiijua discipline
ka kiongozi mwadili nampenda mjinga na mtoaji, 
kitani wanga hunihofia kama bingwa wa uponyaji
linda chako mjinga watu wanawinda wako safi
ukizingua unagongwa tako kama mzinga wa konyagi
nampenda hasa ninayehisi anaijua heshima
daktari rudia darasa mi ni ugonjwa usio na jina
wanashangaa mara dina mara hawa mara huyu we ni buyu mi moko sawasawa?



[MashairiBongoFlava.blogspot.com]

Sign in kutumia Akaunti yako ya Facebook kisha comment!