[Ngwair & JD]
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
[Ngwair]
yoh nyie mademu gani, sikizeni kwa makini
mimi hivi kwanini mnakuwa hamjiamini, yeah
mnajua nyie yaani mna nguvu zaidi ya sisi
mwanaume kwa demu ni kama mfupa kwa fisi
sina nia ya kubadili maadili, sio
nnachopinga nyie kushikwa masikio
sema tu hamjui umuhimu wenu,
ila leo nitawaambia tu ila iwe siri yenu
mi mwenyewe naenda club kila wiki
haina maana huwa nafuata tu mziki
mkiwa wachache huwa naona hapalipi
hata niwe na hela vipi na lundo la marafiki
vijijini asilimia tisini maskini starehe yao ni pombe na nyinyi
sasa mpaka lini mtakuwa mnanyanyasika na kudharaulika
au wenyewe mmeridhika
kuolewa mna haki wala msiite bahati
we unadhani, wanangu mi nitalea na nani?
sema tu wengi ni vicheche
japo sio moto hakuna asiye ogopa cheche
yeah
[Ngwair & JD]
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
[Mwana FA]
mfano mi sifagilii kabisa mitungi
ukiacha mabinti sio mineli sio mirungi
ila nakosa imani nikiwaona mnajigonga
yaani hadhi yenu inashuka kimsimamo mnapoyumba
mmekosa nini kinachofanya msijiamini
au mwalimu wenu kipofu msemo nanyi mnaamini
msichimbe madini sawa
ila sio wote muwe wafanyakazi wa ndani
hesabu hazipandi sioni ngumu kuwa rubani
ila japo karani na imani haishindikani
big up kwa ma mommy, wote ambako mbite imelala kichwani
sisemi mlee wanaume kama mabinti
ila mnapojitosheleza machaguo yanaongezeka
hamuoni, basi someni
kama uliishi vibaya poa wanangu irekebishe
wenye upeo mdogo ndo daima wanakuwa vicheche
kuolewa sio lazima japo inaongeza heshima
ina hadhi yake, hawatajali mke wa kigogo au wa mkulima
na ole wenu mpenda kutafuta vyenu
mnatamani tu vya wenzenu
ndo maana huwa mnamegwa na wazee umri wa babu zenu
nieleweni jikazeni
msipokomaa waume zenu watawaletea vicheche ndani
Niamini, Binamu
B Yeah
[Ngwair & JD]
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
wengine mnapenda sana vya kupewa
ndo maana wengi wenu mnaishia kuchezewa
mnamegwa mnaachwa na hata mkiolewa..
ndoa inajaa visa na kuonewa
mfano ngwair narudi muda ninaotaka
na ukineletea ki'bass tu asubuhi talaka, kwenu
si najua huna kitu, zaidi ya begi lako
ila nisingethubutu endapo nyumba ni yako
najua hamuwezi kuenda haja ndogo mmesimama
ila mna uwezo wa kufanya kila siku mnachofanya
hata kuwa Raisi mwanamke pia ana haki
mradi tu awe na vigezo wanaume tunapata wapi?
kama kusoma wote ruksa kusoma
bado biashara hata ufundi wa kushona
wenzenu wachache bungeni si mnawaona?
hata kuimba imbeni tu msione noma
ka Sista P, Zay B, Stara, Ray C
Je wataka endesha Prado ka Lady Jay Dee?
amini wote tumezaliwa watupu
na huvaa ni kutokana tu na juhudi za mtu
holla
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hata kama sijamaliza, ah sikiliza
yep
[MashairiBongoFlava.blogspot.com]
Sign kutumia akaunti yako ya Facebook kisha comment!