Jay Moe - story za wazi wazi


walikuwa na hamu, na  mawazo arudi vipi tena
Baada ya salaam, mazungumzo ndo mi nnavofanya
..ili, mambo yawe thabiti ili mradi tusipotee njia
Nna story tofauti tatu leo ntakazohadithia

Ya kwanza ni ya Ahmedi
Wengi walimwita meddy,
muuite eddy kama unamuhusudu na ye ndo anavohusudu
Familia, zilijuana miaka nenda miaka rudi
Tangia, hatujaanza soma wala hatujui nini Hood
siwezi sema alinizidi akili enzi za primary
eti kwa maana ye alifaulu mi nikafeli
aliyefeli primary, ndo aliyemaliza Seko
aliyefaulu alishindwa kufika hata cha tatu kidato
Education ma s, dili kushika mishiko
kwenye No akaweka Yes yote kutaka maujiko
Wazazi walipojua walimsema akawa mbishi
wakamwambia kama hutaki kusoma hapa hauishi
Akahamishwa shule, napo baada ya muda akaacha
Kwa kupenda kuishi maisha ambayo muda wake haujafika
akaanza udokozi pale home kwa kujificha
wizi ukazidi nyumnbani mpaka wazazi wakashtuka
akafukuzwa, trust me, alikuwa mzigo kwa wazazi
Akajiingiza rasmi, kwenye mambo ya wizi
Maisha anayoishi hivi sasa utadhani alipewa radhi
Jela miaka tisa kwa kesi ya kupora na ujambazi

alikuwa mtoto wa kishua maisha akayachezea
Jinsi alivyokuja kuwa, hakuna aliyetegemea
Cheki maisha anayoishi sasa anavyosikitisha
Cheki maisha anayoishi sasa anavyosikitisha


/Mariamu alikuwa demu mzuri sana form four yetu yote
eh, nyumbani mambo yalikuwa safi
Ndo kitu ambacho watu wengi walimchukia kutokana na kuringa kwake
Lakini leo hii, maisha yamebadilika huwezi amini/


Mariamu alikuwa mtoto aliyekuwa na uzuri wa peke yake
mimi mwenyewe mmoja wapo kati aliyetaka ajiweke, ili anione mchumba wake
Alisimama peke yake, aliringa kwa uzuri wake tajiri familia yake
Kama h*nyi au hali kwa jinsi alivyojisikia, na vile home kuna mali kiburi alijijengea
Hali iliyofanya wengi wanaomjua kumchukia, tuliosoma naye hio tabia tulishaizoea
Wazazi walisoma, ndo maana maisha yao ya juu,
ye hilo hakuliona cha maana aliona ni usistaduu
Pesa zikamtia udhaifu akaona za nyumnbani hazitoshi
Shuleni akacheza rough, masomo akashindwa pass
alipata zero kitu ambacho wazazi hawakuamini
angekuwa mtoto wa kiume wangeshamfukuza nyumbani
wakaona sio mbaya kama atarudia mtihani kitu ambacho mariam hakikumuingia akilini
wakamuuliza anachotaka, akajibu Computer,
Cheti akapata kwenye stashahada akachemsha
Baada ya kupewa ujauzito inasemekana na kizito
Ambaye ana mke na pia nyumbani ana watoto
Cha moto kikaanzia nyumbani alipofukuzwa
Kumbe yule kizito ana ngoma anafanya kuisambaza
Hakumsikiliza Jose Mtambo alipoimba kizaazaa
Yamemuharibikia mambo na mtoto bado hajazaa

alikuwa mtoto wa kishua maisha akayachezea
Jinsi alivyokuja kuwa, hakuna aliyetegemea
Cheki maisha anayoishi sasa anavyosikitisha
Cheki maisha anayoishi sasa anavyosikitisha

Inno alikuwa mtu ambaye.. usingeweza kutegemea
kwamba leo angekuja kuchanganyikiwa akili
au angekuja kutumia madawa ya kulevya
Ni basi tu, nadhani ni kutokusikiliza la mkuu

siishiwi mifano ya fasihi kweli siishiwi maneno
siishiwi masomo, ya tahadhari tuwe na msimamo
hatua kwa mtazamo, usije ukalikanyaga shimo
Ukabaki humohumo, ukashindwa kutoka kama inno
ali'ignore wazazi walipomsihi ajipange
leo ana ugonjwa wa uchizi na kila siku mirembe
wala sio shauri ya bange poda ndio iliyomchanganya
aliyochanganya wazazi wote mtaani kutupa lawama
sababu walijua si ndo tulikuwa kaka zake
kwahiyo kama tulijua kwa nini habari tusiwape
Yupi anamuuzia kete, yupi anamfanya avute
wazazi walitaka wajue wabaya wakakamate
washafanya kila kitu na bado kijana Mteja
Kwenye familia yake yeye ndo kaka ye ndo mkubwa'
Baba kaishiwa shauku, mama anamuomba mungu
akijiuliza kila siku kafanywa nini mwanangu
anadata akienda milembe akirudi amepona
damu yake ikikosa unga akili yake inakuwa nzima
Tatizo hana stahimili, baada ya miezi miwili utashangaa
yupo maskani na mateja anapata mbili
Mpaka leo ameshindwa kuepuka suala la madawa
Anaendelea kupinda akili yake inazidi pagawa
Unga sio siri anaupenda anakiri kuucha sio sawa
Bora awe mjinga na akili ye na unga kama kawa

alikuwa mtoto wa kishua maisha akayachezea
Jinsi alivyokuja kuwa, hakuna aliyetegemea
Cheki maisha anayoishi sasa anavyosikitisha
Cheki maisha anayoishi sasa anavyosikitisha


[MashairiBongoFlava.blogspot.com]