ni mbali sana ninapotokea, na ninazidi kuja kwa kusonga mbele
oooh
yeah
Namiliki cheupe manga na japo na cheusi dawa
angalab ziki haitaki tajiri hebu twende sawa
ma'bungalow, na magari kama watoto wa bakhresa
kariakoo, kwa muuza duka, nna thamani zaidi pesa
sio muuza sangara, mtaani huniita ghetto professor
uliza dandara, heshima kama dudu kisesa
bongo mnecheza, nyie ni wabongo na hii ndo yenu flavor
mnanipa kiinua mgongo, nashukuru napata fedha
naeza kumbuka niliichoona, nikasahau jina la Movie
naeza, shindwa kusoma kwasababu tu haya maujuzi
kazi yangu mimi ni ku'create tu hizi words
na punch za mkono wa chuma kama mitah or cyborg
naning'iniza MC kama cheni za gold, kwenye kifua cha Pedeshee
najua unanisoma Bwa'shehe
Yo, nna flow cause kuna F kwenye Fid
Ni mwanza coz kuna M kwenye MC
Na who else kwenye B
Niite Ngosha, the Don
Na so James, Japo my words are Bond
Na make dollar ina make sense
Mafala wana'act acheni hayo maswala ya.. kudadadek
Nahitaji respect na si Stress ka K-Arrest
ni mbali sana ninapotokea, na ninazidi kuja kwa kusonga mbele
ni mbali sana ninapotokea, na ninazidi kuja kwa kusonga mbele
oooh [Nna'change rock city kuwa rap city, ona]
yeah
Natabasamu hata kama nna njaa, niheshimu
kama Rhymes ni majungu, kweli ufalme ni wa jamaa
historia hujirudia sio sana kama movie za champlain
amani kwa ma mcee na ma'produce wazuri wa sampling
niko na customers, sihitaji kuwa-hassle
naenda nao ngazi kwa ngazi, nkileta u'snitch watani'rasco
siogopi kukosea ndo maana wananiita mbunifu
nazidi, kuendelea, napakua hits kila siku
nasema, naongea, natema vitu viko deep
mapema nliiacha kuongea na zingine nge'ongea ingekuwa sio ishu
nachukia kukosea, na siwezi furahia kupotea
kimbia nnapotembea ka unataka kunifikia
na pia, mi sina spare kama unavyoniskia
najua, vile unionavyo sivyo ulivyonihisia
sijachagui, kama ombaomba kwa dua inaeza jikomba
na ikamgusa, hata ukiweka ukuta ka mjomba
mnajiuliza mi nani, nawajibu mi ni mtu fulani
msome kitaani nani anasema akomi nami?
wapinzani siwaoni, mliopo gizani njooni kwa mfalme
mnayoyafanya ndotoni mi nayafanya hadharani
yaani niliyoyafanya utotoni nyie ndo mnayafanya ukubwani
ni mbali sana ninapotokea, na ninazidi kuja kwa kusonga mbele
ni mbali sana ninapotokea, na ninazidi kuja kwa kusonga mbele
oooh
mbali sana, ninapotokea,
kuna mvua jua kali pia
Ghetto kibao
yeah
Ghetto kibao
uh uh
{Akiongea: .... i guess they dont understand, this is the king of the motherland, and just for the record, naomba mjue, rock city hiphop is back and runnin..' at full power!}
[Mashairibongoflava.blogspot.com]