Mwana Fa, Linah - Yalaiti




Sshhhh,classic classic..
Keeping the good music alive,
That’s me job,
You my sunshine my moonlight and everything I dream about,
Linah
let’s go..


Yalaiti,napenda pasi kifani
Tofauti,sikutilii moyoni
Sikuachi,leo na kesho peponi
I I I I , I love you

Yalaiti,napenda pasi kifani
Tofauti,sikutilii moyoni
Sikuachi,leo na kesho peponi
I, I, I, I, I love you


Sambaza love kama dawa
huachi mpaka napagawa
hata ukisema mi sio Hamis natingisha kichwa
mapenzi yako yanielemea ka chupa nzima ya tequila
usirushe somo nakupenda acha masihara
ina haja gani unishikie fimbo ili nikuskize ka gorilla
mi ni mtu na mapenzi yangu nishaacha zamani usela
una matatizo najua,na mi nna yangu boo
we sit together from this moment,we see them through
nikikukosea nisute,nipige vibao,nizodoe
ninunie kwa siku kadhaa ila nnachoomba usinikimbie
mapenzi ya utemi kwangu hadithi mambo ya kizamani hayo
ukiniudhi ntapiga kwa khanga ndio nimefunzwa tanga hivyo
utaoga mabusu nikufute kwa kumbatio mpaka kama nikisafiri ukinikumbuka iwe kilio
sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe.. B

.
Yalaiti,napenda pasi kifani
Tofauti,sikutilii moyoni
Sikuachi,leo na kesho peponi
I, I, I, I.. I love you

Yalaiti,napenda pasi kifani
Tofauti,sikutilii moyoni
Sikuachi,leo na kesho peponi
I, I, I, I.. I love you

Nshasema sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe
ushaangaliwa niunge tela usingoje mpaka uambiwe
we ushaangukiwa anguka nawe usizubae mpaka irejewe
kwako ntakuwa Bushoke sitajiuliza ka zezeta
yetu yawe mahaba mapenzi zamani tumepita
mi sakafuni we ukingoni mbio zangu haziendi mbali
una moyo wangu ntapenda bila kujalihata marefa wana timu zao mama panga matokeo
pambano lianze najua goli ngapi ngapi leo
usiache kuvaa nguo ndefu hivi vimini achia vicheche
mwanamke kwetu staha tunaovipenda sio wote
akili haziuwezi moyo na wenyewe una ubongo pia
hauwezi ukafuatafuata kila utakachouambia
nitajiwapo mapenzi naipata picha yako kwanza
natamani uipate yangu na iwe inakuliwaza

Linah..
Toa shaka na wasiwasi moyoni
Toa shaka na wasiwasi moyoni...mashallah
Kukuepuka hilo haliwezekani
Takushika,leo na kesho peponi Yalaiti,napenda pasi kifani
Tofauti,sikutilii moyoni
Sikuachi,leo na kesho peponi
I, I, I, I.. I love you

Yalaiti,napenda pasi kifani
Tofauti,sikutilii moyoni
Sikuachi,leo na kesho peponi
I, I, I, I.. I love you