simba dume nyama ume pori mwendo kama mfalme
anaheshimika anapopita anaogopeka zaidi ya vita
kamanda wa afrika wataliwa na kushuka
cha kwanza wanamtafuta
kumuona simba ndo hasa kilichowaleta
japo hawamli nyama hawampandi mgongoni
labda iwe kwenye sinema
lakini bila simba, ham, bila huyu mwamba kwa mtalii hatoridhika
na huenda asione maana hata ya kuja afrika
sasa kama simba alivo mbishi ndo mimi navoishi
ye anawinda kwenye msitu mi nalinda mziki wetu
wakati simba anawinda ilimradi apate nyama
mimi mziki naulinda kusudi nipate heshima
simba bila nyama niwaza kufa njaa
hata mimi bila heshima ningekosa motokaa
simba iwindi ili alinde
yes ni kama mimi siwapondi ili mradi niimbe
simba anawinda ili ashibe
basi ndo kama mimi nawaponda game ibambe
mbona unaandika uzembe
hilli simba dume, king of the Jungle au ngurume [Cheza Nani?]
hilli simba dume, king of the Jungle au ngurume [Cheza nani?]
Simba dume linang'ata, [ham]
Simba dume linang'aata, [ham ham]
Simba dume linang'ata [Ham]
Simba dume linang'aata [Ham ham ham ham]
Kama simba anavowinda msituni bila kelele
basi ndo kama mimi ntavoilinda hii fani mpaka milele
simba kama simba wala hafanani na Swala
hata mimi kwenye kuimba sifanani na mafala
kwanza siuzi sura, pili sionekani kila mara
yaani kama mbugani jinsi unavomuona swala
hata kando ya barabara unamkuta anakulakula tu
kumuona simba porini mpaka umsake
machimbo yake ukimuona barabarani basi ana safari zake
ndo kama mimi japo moro ndo nyumbani
ila usidhani kwamba ukifika utaniona njiani
nashangaashangaa, labda unifate maskani za mjani
simba dume anaonekana wakati wa kwenda kuwinda
hata mfalme naonekana wakati wa kwenda kuimba
napenda nyumbani kama simba anavopenda kichakani
hafanani na manyani kutwa kucha yako njiani tu
ndo kama mimi sifanani na fulani usiku kucha viwanjani
msanii akirudi nyumbani unadhani ataandika nini zaidi ya stori za chumbani
hilli simba dume, king of the Jungle au ngurume [Cheza Nani?]
hilli simba dume, king of the Jungle au ngurume [Cheza nani?]
Simba dume linang'ata, [ham]
Simba dume linang'aata, [ham ham]
Simba dume linang'ata [Ham]
Simba dume linang'aata [Ham ham ham ham]
haha kama zamani sio
toka Bongo rekodi
king wa ma-bongo fleva
sele msundi
king wa bongo forever
Yaas na kize feruzi waelekeze
vijana wamekosa heshima (sana)
bado hawajanenwa
bado hawajachezwa ngoma
wanatamani kuitwa mama kabla hata ya utu uzima (hawana maana)
wanaupotosha uma, afu wanang'ata chuma
yaani mbao wanajaribu kuitafuna
wanadanganyana, wanawanga mchana
wanadhani simba kama mbwa hakung'ati ukimjua jina
kwetu hilo hapana
mtakufa huku mnajiona wana
ham (mcheza nani)
Ham ham ham ham (Mcheza nani?)
/