Polisi wana'support gansta rap, ili uhalifu uongezeke!
wabana pua kuimba mapenzi je itafanya ukimwi usepe?
media zinapromote beef wanadai zinakuza mziki!
wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
hizi ni propaganda usiulize ninani ni yupi saa ngapi ilikuaje nanani... ili iweje?
hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza Blunder
(Yule last king of scotland sio Idd amini wa Uganda)
machungu unapozimwa ili ufunikwe na asiyeweza
mbaya zaidi wanampa promo lakini kwenye show nnammeza
hautaki kuwa tatizo sababu unaeza tatuka
huezi jua wapi ntatua ka jiwe gizani likitupwa
wanaficha ili nisione wakati tayari nishajua
hamkomi? igeni nione jinsi msamba mnaupasua
hivi unaishi ili ule? au unakula ili uishi?
kumbuka, a small leak will sink a ship
mazingira hatarishi mabwana afya wanapesa mob..
uswazi tunaomba mvua zinyeshe ili tutapishe vyoo
ugopa kuoa haraka kama unaogopa talaka
na uki vote in a hurry ujue una'produce corruption
maneno yao ni matamu lakini midomo yao inanuka
ukipewa usisahau ukitoa toa bila kukumbuka
usihofie kupitwa ili mradi muda haukuachi
amini kesho itafika kama ipo ili uipate
tunachukiana kwasababu tunaogopana
tunaogopana kwasababu hatujajuana
hatujuani kwasababu tunatengana
dunia ni nzuri walimwengu hawana maana
Polisi wana'support gansta rap, ili uhalifu uongezeke!
wabana pua kuimba mapenzi je itafanya ukimwi usepe?
media zinapromote beef wanadai zinakuza mziki!
wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
hizi ni propaganda usiulize ninani ni yupi saa ngapi ilikuaje nanani... ili iweje?
hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza Blunder
(Yule last king of scotland sio Idd amini wa Uganda)
Polisi huniita mzururaji na wanajua mie ni Mc
Kisha hunipa ishara kama wanavuta uradi kwa tasbii
baya lisilonidhuru ni jema lisilo na faida
nashukuru kote nasikika napotoa haya mawaidha
kuanzia kata, tarafa wilaya mikoa hadi ngazi ya taifa
nikifa, siachi scandal nauhakika ntaacha pengo
kwa hivi vina hata wakulima hujikuta wanameza mbegu
pia ni kama liberation struggle machoni mwa Che Gu..
ukiwa mkali kama maco chali raia atafeel tu
wajinga ndo hufa kwa wivu sababu hawako real tu
rafiki sio urafiki usipochanganywa na kazi
mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi
haupaswi kumuamini muongo hata kama akiongea ukweli
ni dhambi kutumia dini kama njia ya kutapeli
wanajiingizia kipato kwa kivuli cha misaada
hawatufunzi tuwe viongozi labda viongozi wa kuwafuata
utata huja tunapoanza kuwachunguza
badala ya kuwafuata ndipo siri zinapovuja
tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga
ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda
kama umevutiwa na asali jiandae kumkwepa nyuki
hauwezi kumtisha kwa mawe adui aliyeshika bunduki
ni uchunguzi tu wa kisayansi ambao haukufanikiwa
kama ng'ombe kula nyasi tu halafu anatoa maziwa