Diamond - Nitarejea

aaaah

vipi mizigo umeshaweka tayari(mmh, aha)
nsijechelewa nkaachwa na gari (mmh aha)
Basi jikaze usilie mupenzi (ahaaaa)
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi (ahaaa)
Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna
Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma, sema ntafanya nini na pesa sina
nakuonea na huruma, bora niende mjini kusaka Tumaa!

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea

nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

wanajua kwamba nafsi na roho
vitakuwa na wasiwasi
ukumbuke na moyo utajawa na simanzi
ntakapokuwa nakwenda shambani
afu niko peke yangu honey
ntapokuja kuwa na majirani ntaaumia aaah
pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani
sina wakunitua nyumbani ntaliaa aaah

maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo
hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo
vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh
we niombee niepushwe na balaa na maradhi ohh
eeeeh

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi
usisahau kama mkeo na wana, umetuacha na dhiki

vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki
wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi
Kumbuka mkeo na wana nyumbani, umetuacha na dhiki ohhhh

vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki
wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

ntarejea mama
niombee nirude salama
ohhh watoto wadanganye iiihhhhh, uhhhhhh